Burudani ya Michezo Live

Maua Sama awataja wapishi wa Main Chick

Maua Sama amefanikiwa kuwa msanii anayefyatua hits baada ya hits.

Kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake Main Chick. Lakini siri ya kuwa na uwezo wa kutengeneza vigongo, ni utayari wake wa kushirikisha vichwa vingine vyenye uwezo mkubwa katika kuandika nyimbo.

Kwenye interview na TBC Taifa, Maua amesema alikuwa studio kurekodi wimbo wimbo huo lakini akahisi anaimba kitu kile kile na hivyo kuamua kuita jeshi kumsaidia.

“Kwahiyo nikampigia simu Ibrah Nation pamoja na Tommy Flavour, wakaja pale wakanisaidia kupata maneno ndio yote hayo yanayosikika kwenye wimbo, wao wamehusika katika asilimia 70 kuhakikisha nyimbo inakaa sawa,” amesema Maua.

Mtazame zaidi hapo juu akiuelezea wimbo huo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW