Burudani

Maurice Kirya ashinda tuzo ya RFI

Kundi la Majaji wakiongozwa na msanii wa Hip Hop nchini Ufaransa, Passy, wamemchagua kwa kauli moja Maurice kirya 27 kuwa mshindi wa tuzo za ‘RFI Discoveries Music Awards’ kama msanii bora anayeibukia.

 

Maurice kirya aliweza kutwaa tuzo hiyo mbele ya Winyo kutoka Kenya na Lexxus regal kutoka DRC Congo na wengine ambao ni pamoja na Ay (Tanzania), Bholodja (Swaziland), Elie Kamano (Guinea-Conakry), Koppo (Cameroon), Lexxus Regal (DRC), Mao Otayekc (Cote D’Ivoire, Sandra Cordeiro (Angola), Smokcey (Burkina Faso) and Winyo (Kenya).

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo radio France International Maurice alichaguliwa kuwa mshindi wa jumla kutoka katika kundi la washiriki 500 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha ikumbukwe kuwa Ay ndiye alikuwa mshiriki pekee toka Tanzania katika kinyang’anyiro hicho.

Akiongea na mwandishi wa Bongo5 kutoka Kampala nchini Uganda ilipo makazi yake msanii Maurice alisema alishindwa kuamini na kukosa maneno baada ya kupigiwa simu na kuambiwa ameshinda tuzo hiyo. “ Kwa kweli sina cha zaidi cha kusema kwani nimefarijika na kufurahi sana.’.

Haya ni matunda ya kazi na jitahada kubwa niliyofanya na kuiweka katika muziki huu, naahidi kutumia kila liwezekanalo ili nijitolee kwa hali na mali kufaidika na ushindi huu.

Tuzo hiyo inakwenda sambamba na fedha taslinu euro elfu saba sawa na shilling million 14 za kiTanzania na inafungua milango ya kujitangaza kwa kijana huyo katika jukwaa la kimataifa. .Msanii huyo ataanza kuzunguka dunia kama sehemu ya zawadi ya kituo cha Radio France International.atafanya onyesho jijini Paris na Djamena nchini Chad kabla ya kuanza kazi ya kfanya maonyesha barani Africa.

Pia msanii Maurice kirya atapata euro za ulaya 11,000 kama sehemu ya pesa kwa ajili ya kukiendeleza kipaji chake. Tuzo hizo za RFI zimekuwa mfano bora wa tuzo za wasanii duniani kote ambapo waandaaji, Radio France international wanashirikiana na Sacem, Utamaduni france, Wizara ya Ushirikiano wa kimataifa ulaya  na ufaransa na jumuiya ya nchi zinazozungumza kifaransa.

Akiongezea maneno kutokana na kutunukiwa tuzo hiyo Maurice alisema “ Hii ni nafasi yake yeye kuzunguka duniani na kuuelezea muziki wake vizuri. Pia alichukua nafasi hiyo kuwashukuru wapenzi wake wa muziki nchini Uganda. ‘Ukiangalia televisheni utaona nyimbo za afrika magharibi na Kusini lakini afrika Mashariki ambako kuna wasanii wengi wenye vipaji hawaonekani’,alisema msanii huyo.

Alimalizia kwa kusema hii ni nafasi kwa wale wote wanaopigania mafanikio yetu hasahasa watu wangu wa nyumbani Uganda. Nataka kuwathibitishia kwamba tunastahili kutambulika kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents