Burudani

Mauzo ya tiketi za pambano la Mayweather Jumamosi hii yadoda

Mauzo ya tiketi za pambano la Floyd Mayweather Jr na Andre Berto Jumamosi hii yamedoda.

Mayweather-Berto-Poster

Tofauti na pambano lake lililopita dhidi ya Manny Pacquiao miezi minne iliyopita, tiketi za pambano hilo zimeendelea kupatikana kirahisi.

Mayweather aliingiza zaidi ya dola milioni 200 kwenye pambano na Pacquiao.

Katika pambano la Jumamosi hii, Mayweather ataingia dola milioni 32.

Pambano hilo litachezwa kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena.

Berto ameshindwa mapambano matatu kati ya sita aliyopigana mwishoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents