Mawakala wa Benki ya NMB wapewa elimu kujiepusha na utakatishaji fedha

Benki ya NMB imetoa mafunzo maalum kwa mawakala wake kuhusiana na namna ya kuzuia utakatishaji fedha; na pia mbinu za kuzuia kufadhili shughuli za kigaidi.

 Mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na Arusha, ni utekelezaji wa maagizo ya Benki Kuu (BoT) kuhakikisha mawakala wa benki hawawi sehemu ya kutakatisha fedha zinazopatikana kwa njia zisizo halali.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Wakala – Bw. James Manyama alisema ili mawakala hao kutotumika vibaya hawana budi kuzingatia sheria na kanuni za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu ili kushirikiana na Serikali katika kukomesha vitendo hivyo.

Mawakala kutoka Manispaaa ya Temeke wakiwa katika mafunzo ya jinsi wanavyoweza kuzuia utakatishaji fedha

“Ni wajibu wetu kama Benki kuwaelimisha mawakala wetu kuwa makini wakati wote hasa kwa wateja ambao
wameshajenga ukaribu na mazoea nao. Pia ni muhimu kuwa makini na wateja wanaoweka fedha nyingi na kisha wanazitoa ndani ya muda mfupi, na ukiangalia kiasi hicho cha fedha wanachoweka hakiendani na maisha yao. Inapotokea hali hiyo wanapaswa kutoa taarifa sehemu husika,” alisema James.

Christine Mwidunda, ambaye ni Meneja wa Mawakala NMB, alisema vyanzo vya fedha haramu ni kama vile
ukwepaji wa kodi, biashara zilizopigwa marufuku zikizemo dawa za kulevya, usafirishaji wa silaha na binadamu, ugaidi na utekaji n.k.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW