Habari

Mawaziri 10 waambukizwa corona Sudan Kusini, Wote waliambukizwa na mjumbe mmoja

Mawaziri 10 wameambukizwa virusi vya corona nchini Sudan Kusini, msemaji wa serikali ameithibitishia BBC. Waziri wa Habari wa Sudani Kusini Michael Makuei ameiambia BBC kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na corona nchini humo.

Katika mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hajakutwa na maambukizi.

Inaripotiwa kuwa mawaziri hao wamepata maambukizo baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona.

Mawaziri wote 10 wamejitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya.

Taarifa za kuambukizwa kwa mawaziri hao zinakuja siku chache baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar kutangaza kuwa amekutwa na virusi pamoja na mkewe, ambaye ni Waziri wa Ulinzi.

Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo wamekutwa na virusi na kwa sasa wapo karantini.

Mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kupata corona Sudani Kusini, huku watu wane wakipona na sita kufariki.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya hatari ya kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya wan chi hiyo ambao una uwezo mdogo kutokana na mgororo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambao umeathiri ustawi wa maendeleo.

Kwa sasa rais Kiir wameweka tofauti zao za kisiasa pembeni na kutengeneza serikali ya umoja wa kitaifa, japo hawajaweza kukubaliana katika baadhi ya mambo ya msingi kama udhibiti wa majimbo.

Wakati corona ikiendelea kuleta wasiwasi, nchi hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa chakula kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents