Habari

Mawaziri msitoe matamko yasiyotekelezeka – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikalini.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ni vema viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents