Habari

Mawaziri msiyatumie madaraka kujitajirisha binafsi – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa huku akiwataka kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo Jumatatu hii, alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

“Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha alisema Mawaaziri na Manaibu Waziri wazingatie Katiba ya nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa majikumu yao ya kila siku.

Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hata hivyo Waziri Mkuu aliwaagiza Mawaziri wahakikishe wanakwenda kufanya ufuatiliaji wa tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao.

Waziri Mkuu jana hiyo hiyo amesafiri kuelekea nchini Canada kwaajili ya shughuli za kikazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents