Habari

Mawaziri na wabunge watoro wachimbwa mkwara

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameonya kuhusu kuwepo ongezeko la wabunge na mawaziri watoro bungeni.

ndugai-1

Amesema Ijumaa hii wakati wa kuahirishwa kwa bunge mjini Dodoma.

“Kuna orodha nimeiandaa ya watoro katika kamati, lakini kwa leo sitawataja hapa kwa sababu nimeona tuendelee kuwafuatilia katika vikao vijavyo, kama hawatabadilika nitawaambia waajiri wao, yaani wabunge watoro nitawasema kwa wananchi wao na kwa viongozi wa vyama vyao na kwa mawaziri watoro, nitamwambia namba moja, kwamba mawaziri hawa hawawajibiki ipasavyo,” alionya Ndungai.

Alisisitiza kutotania katika suala hilo na kuongeza kuwa mahudhurio katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 unaotarajiwa kuanza Novemba Mosi mwaka huu, ndio kitakakuwa kipimo chao cha mwisho.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents