Habari

Mawaziri washuhudia kifo cha mgonjwa wa RVF

MANAIBU Mawaziri watatu jana walianza ziara katika Hospiali Kuu ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya Mirembe, huku wakishuhudia mgonjwa mmoja akifariki dunia kwa kudaiwa kuwa na Homa ya Bonde la Ufa (RVF).

Martha Mtangoo, Dodoma

 

MANAIBU Mawaziri watatu jana walianza ziara katika Hospiali Kuu ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya Mirembe, huku wakishuhudia mgonjwa mmoja akifariki dunia kwa kudaiwa kuwa na Homa ya Bonde la Ufa (RVF).

 

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Charles Mlingwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani watatembelea wilaya zote na maeneo yote yaliyoathirika na ugonjwa huo.

 

Katika ziara hiyo katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya Mirembe jana, mawaziri hao walitembelea wodi ambazo zina wagonjwa hao ambapo katika wodi nne jumla ya wagonjwa 40 walitembelewa.

 

Wagonjwa wawili walifariki dunia jana asubuhi na mmoja alifariki dunia mchana akishuhudiwa na mawaziri hao.

 

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda alisema hadi kufikia jana wagonjwa watatu walikuwa wamefariki dunia, wawili kati yao ni waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mirembe na mmoja kutoka katika Hospitali Kuu ya Mkoa.

 

“Kwa mujibu wa saa zetu za kitabibu tunasema wamekufa wawili kwa kuwa huyu aliyefariki dunia sasa hivi mchana yaani baada ya saa sita tunahesabu amekufa katika siku nyingine mpya na ripoti yake itatolewa kesho (leo),” alisema Dk. Kigoda.

 

Dk. Kigoda alisema wanafanya ziara hiyo kwa muda wa siku saba na baadaye watatoa taarifa juu ya hali ambayo wameiona katika maeneo ambayo watatembelea. Naye Dk. Mlingwa alisema yeye kama Waziri wa Maendeleo ya Mifugo hafurahii kuona mifugo yake kwa sasa hailiwi jambo ambalo linashusha mapato ya serikali

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents