Michezo

Mayweather amfuata McGregor katika karate

Mwanamasumbwi nchini Marekani, Floyd Mayweather ameamua kulifanyia kazi wazo lake la kuingia katika mapambano ya karate ‘mixed martial arts’ mchezo ambao hutumia viungo vyote vya mwili badala ya kutumia mikono pekee.

Mayweather amelithibitisha hilo baada ya hapo jana siku ya Jumanne kuposti picha zake na kipande cha video kinachomuonyesha akiingia katika ulingo wa mchezo huo.

Kiongozi huyo wa timu ya The Money aliposti kipande hicho cha video bila kuandika kitu chochote ikiwa ni kama ishara ya kuingia katika mchhezo huo.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 alirejea katika mchezo wa masumbwi baada ya kupigana na McGregor na kushinda katika pambano lake la 50 pasipo kupoteza hata moja.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents