Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mayweather amshangaza McGregor kuzipiga na kijana wa miaka 20, ‘Kama naingiza dola Mil. 300 kwa sekunde kwanini ishindikane’

Bondia machachari wa UFC, Conor McGregor ameshangazwa na maamuzi ya Floyd Mayweather hapo jana siku ya Jumatatu kutangaza kupambana na kijana wa miaka 20 raia wa Japan, Tenshin Nasukawa.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, McGregor ameandika maneno makali mnoo yanayomhusu Floyd baada ya kutangaza rasmi kuzipiga na mpambanaji huyo wa ‘kickboxer’, Tenshin Nasukawa.

”Hiyo ni ‘tracksuit’ au ‘sauna suit’ Floyd hahaha, hivi kuna habari gani hapa Tokyo ?, haya kweli ni mabadiliko ya hali ya hewa wala siyo masihara,” amesema McGregor.

Conor McGregor ameongeza ”Ujinga gani unaendelea hapa ?, ni nani huyu dogo unayekwenda kupigananaye ?, huu ni uwendawazimu,” hayo ni baadhi ya maneno mache tu kati ya mengi aliyoandika ambayo yanaonyesha kumdharau na kumkejeli Meywether kwa maamuzi yake ya kutangaza kupigana na Nasukawa ambaye umri wake wa miaka 20 ni mara mbili na aliyokuwa nao yeye.

Floyd Mayweather is to fight Japanese kickboxer Tenshin Nasukawa on New Year's Eve

Lakini kauli hizo ni kama zimejibiwa na ‘Money’ kwakuwa wakati akitoka kupambana na bondia huyo Floyd alisema kuwa kwenye mchezo wa masumbwi hakuna alichobakiza hivyo anachotazama kwa sasa ni fursa ya kuingiza mkwanja na inapojitokeza hakuna kinachoshindikana.

”Tunafanya mambo ya kijinga wakati mwingine, lakini mimi siyo miongoni mwao. Kama naiyona fursa ya kutengeneza dola milioni 300 (kama bilioni 686 za Tz) kwa sekunde kwa nini nisipigane,” kauli hiyo imekuja mara baada ya Mayweather ‘Money’ kupigana na McGregor huko Las Vegas.

Mayweather has signed with Japanese MMA promotions company RIZIN Fighting Federation

Mayweather mwenye umri wa miaka 41 amepigana mapambano 50 bila kupigwa hata moja huku mwishoni akionekana kupigana na McGregor baada ya kutangaza kustaafu.

Hata hivyo bondia huyo tayari amesha ingia saini na kampuni inayosimamia ngumi za ‘martial arts’ ya Japanese mixed martial arts promotions company RIZIN Fighting Federation, ingawaje bado haijafahamika mpaka sasa ni sheria zipi zitatumika kwenye pambano lake dhidi ya kijana huyo wa miaka 20,Nasukawa in Saitama.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW