Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mayweather aomba kutumia ‘gloves’ laini amtoe ngeu mpinzani wake

Mbwembwe za kuelekea mpambano wa masumbwi baina ya bondia raia wa Marekani, Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor’s zimevuka mipaka huku zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya mchezo huo kupigwa.

Mayweather ambaye ni mtoto wa bondia wa zamani wa Marekani, Floyd Mayweather Sr hapo jana ameiomba Kamati ya Mashindano ya Ngumi Nevada (NAC) kutumia glovu nyepesi kwenye pambano lake dhdi ya mpinzani wake, McGregor litakalofanyika Agosti 26.

Mayweather na McGregor walitakiwa kuwasilisha vifaa watakavyotumia siku ya pambano na Kamati ya Mashindano lakini badala yake siku ya Jumanne Pretty Boy kama jina la utani wanavyomuita akaomba kutumia glovu zenye uzito mdogo 8oz ili kumpatia maumivu makali mpinzani wake.

Kamati hiyo ilisema kwa mujibu wa NAC kila pambano lina glovu za uzito wake, hivyo suala la kupunguza ukubwa wa glovu hizo linahitaji mjadala ambao utapatiwa ufumbuzi wiki ijayo.

By Hamza Fumo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW