Mayweather na McGregor wavimbiana mitandaoni

Imepita miezi mitano tangu Conor McGregor alipodondoshwa katika mzunguko wa 10 na Floyd Mayweather, lakini bifu lao halionyeshi ishara ya kupungua.

Mayweather alistaafu kwa mara ya pili katika pambano lake na McGregor. Huku McGregor akifanya kila mtu kumsubiri yeye kurudi ulingoni , wawili hawa wanaendelea kutumia vyombo vya habari vya kijamii kujigamba dhidi ya mwenzake .

Jumatano, Mayweather aliweka picha kwenye Instagram ikionyesha jinsi alivyomtungua McGregor katika pambano lao


Na McGregor hakupoteza wakati naye akatuma picha ya kujigamba

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW