Burudani ya Michezo Live

Mayweather: “Nataka kupigana Mchana Khabib usiku Conor, Pambano lililopita sikufanya mazoezi nilipiga pushup tu”

Mayweather: "Nataka kupigana Mchana Khabib usiku Conor, Pambano lililopita sikufanya mazoezi nilipiga pushup tu"

Mbabe wa ndondi duniani kwenye uzito wa kati kutoka nchini Marekani  Floyd Mayweather ambaye alistaafu lakini ametangaza kurejea kwenye ndondi tena akitarajiwa kupambana na Conor McGregor pamoja na mkali kutoka Urusi Khabib.

Ikiwa anajiandaa kupigana na Conor alipata nafasi ya kuongelea pambano lake lililopita kati yake na Conor na kusema kuwa kipindi hicho hakufanya amzoezi kabisa ingawa alifanikiwa kushinda mchezo huo.

Floyd ameongeza kuwa ‘Kitu pekee nilichofanya ilikuwa ni kupiga pushups na situps. hayo ndio niliyofanya kujiandaa na pambano.

Kingine pia nilipiga bags mara kadhaa na situps, Kwa sababu, kwa kweli, kambi za mafunzo zilikuwa katika maeneo tofauti tofauti’,

Nilifanya mazoezi huko Vegas siku chache tu. Wakati mwingine sikuenda kabisa kwenye mazoezi kwa wiki kadhaa. ‘Niliichukua serious Kama nilivyosema hapo awali, nilitaka kufurahia pambano langu nikiwa ulingoni pia Nilitaka kuwaburudisha watu wangu ‘

Ikumbukwe kuwa pambano la mwisho la Mayweather lilikuwa kati yake kickboxer wa Kijapani Tenshin Nasukawa kwenye usiku wa Mwaka Mpya mnamo 2018.

Mbali nahilo Floyd Mayweather Amedai Atapigana na Khabib Nurmagomedov Na Conor McGregor katika Siku Moja!


Upo wezekano wa Floyd Mayweather kupambana na nyota wa UFC (Khabib na McGregor) kwenye pambano la ndondi ndani ya mwaka huu lakini ameweka wazi anataka kuwakabili wote wawili, katika siku moja!

Mwisho wa mwaka jana Mayweather alithibitisha kwamba anatarajia kurudi ulingoni tena mwaka huu baada ya kustaafu na atashirikiana na Dana White (Rais wa UFC) ili Mapambano hayo yafanyike.

“Khabib mchana na Conor wakati wa usiku. Unalipa kiingilio kimoja, labda $ 250 (Tsh 570K), na unapata mapambano mawili.”-Mayweather

Ikumbukwe Khabib atakabiliana na Tony Ferguson mwezi Aprili, kwenye UFC 249, pambano la mkanda wa lightweight, na rais wa UFC White amedai lazima pambano la marudiano kati ya Khabib na McGregor liko kwenye kadi ikiwa Khabib atashinda.

2020 Unaweza kuwa mwaka mkubwa ukiwashirikisha Mayweather, McGregor na Khabib, lakini ni vigumu kuona mapambano yote yakifanyika kwa siku moja tu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW