Michezo

Mayweather vs McGregor kuzipiga kesho

Homa ya mtanange wa masumbwi baina ya bondia, Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor unazidi kupamba moto ikiwa imesalia siku moja kabla ya mchezo huo kupigwa.

Kuelekea katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi usiku bado swala la ni aina gani ya glovu zitatumika katika mchezo huo limekuwa tata hii nikutokana na maombi ya bondia hao kila mmoja kuomba kuvaa zenye uzito mdogo 8oz ili kumpatia maumivu makali mpinzani wake.

Swala la kuamua sasa juu ya vifaa hivyo limeachwa kwa timu za wapiganaji hao kuamua wenyewe.

Mayweather aomba kutumia ‘gloves’ laini amtoe ngeu mpinzani wake

Mpaka sasa bondia, McGregor haja weka wazi juu ya maamuzi yake kama anaafiki kuvaa glovu hizo zenye uzito mdogo 80z au laa wakati kwa upande wa pili wa shilingi Meneja wa Mayweather, Leonard Ellerbe amekiambia chombo cha habari cha Sky Sports kuwa nijambo muhimu la kulitolea maamuzi kwa sasa.

Kamati ya Mashindano ya Ngumi Nevada (NAC) imeridhia kutumika kwa glovu hizo na tayari imeshakabidhiwa ya bondia McGregor ingawa kwa upande wa Mayweather haijajulikana.

Fahamu kilakitu kuhusu mpambano huo HAPA

“Tunauhakika kilakitu kitakwenda kama kilivyopangwa”, amesema meneja wa Mayweather, Ellerbe.

“Kutumia glovu zenye uzito 80z kuna faida kwa pande zote kwa sababu itaongeza uwezekano wa mtu kushinda knockout na ndiyo hasa mashabiki wanachohitaji kukiona”.

Mayweather atapambana na bingwa wa UFC Conor McGregor katika ukumbi wa T-Mobile Arena  hapo kesho huko Las Vegas.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents