Aisee DSTV!
SwahiliFix

MAZISHI YA MUGABE: Familia na Serikali wamaliza mvutano wa mahala atakapozikwa 

Familia ya rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe imekubali kiongozi huyo azikwe kwenye makaburi ya mashujaa wa kitaifa mjini Harare.

Image result for Zimbabwe, Robert Mugabe funeral

Hata hivyo, tarehe rasmi ya kuzikwa kwake bado haijawekwa wazi. Msemaji wa familia ya Mugabe Leo Mugabe amewaambia waandishi habari kwamba machifu wa kikabila katika eneo alikozaliwa Mugabe ndiyo waliofikia uamuzi huo.

MAZISHI YA MUGABE: Familia yake na Serikali vyaingia kwenye mvutano mkali

Leo ambaye ni mpwa wa Mugabe amesema mazishi hayo yatakuwa ya kifamilia na wanaendelea kujadiliana kuhusu siku atakayozikwa kiongozi huyo wa zamani. Mugabe alifariki dunia wiki iliyopita nchini Singapore akiwa na miaka 95.

Image result for Zimbabwe, Robert Mugabe funeral

Familia yake na rais Emmerson Mnangagwa, aliyekuwa mshirika wa Mugabe walijikuta wakivutana kuhusu wapi atakapozikwa Mugabe baada ya mwili wake kuwasili nchini humo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW