Burudani

MAZISHI YA MUGABE: Familia yake na Serikali vyaingia kwenye mvutano mkali

Familia ya mzee Mugabe na Serikali ya Zimbabwe zimeingia kwenye mvutano mkali kuhusu ni wapi mwili wa mzee Mugabe utaenda kuzikwa.

Image result for mugabe body in harare

Serikali inataka mwili wa Mzee Mugabe uzikwe katika makaburi ya mashujaa wa taifa hilo, Huku Wanafamilia wakitaka mwili wake uzikwe kijijini kwake, Kutama nje kidogo ya Jiji la Harare.

Rais wa Taifa hilo, Emmerson Mnangagwa pamoja na viongozi wake wamejadiliana mwili wa Mugabe uzikwe kiheshima katika eneo la makaburi ya mashujaa jijini Harare.

Familia hiyo imetoa taarifa iliyosomeka, “Tumetambua kuwa kuna ratiba ya Serikali ambayo hatujashirikishwa wanafamilia, Serikali ya Zimbabwe inavyoratibu mpango wa mazishi ya marehemu, Robert Gabriel Mugabe pasi kuishauri familia yake marehemu ilio na jukumu la kuwasilisha maombi yake ya mwisho kuhusu mazishi yake, Sisi tutamzika kijijini kwake kama alivyotuachia kabla ya umauti,“.

Viongozi mbali mbali nchini humo akiwemo Waziri wa Elimu nchini humo, Paul Mavhima amesema Mzee Mugabe anastahili kuzikwa kama shujaa wa kitaifa na msiba huo sio wa familia bali ni wakitaifa.

Mtu muhimu wa aina hiyo, ambaye mazishi yake yatahudhuriwa na zaidi ya viongozi 50 wa taifa na wa zamani. Muasisi wa taifa hili hakupaswa kuwa na majadiliano ya hilo. Hakupaswa kuwa na mzozo wowote. Uamuzi unapaswa kuwa wa wazi, anastahili kuzikwa katika makaburi ya kitaifa,”ameeleza Mavhima kwenye mahojiano yake na BBC.

Itakuwa ni makosa makubwa kuwa na mpiganiaji uhuru wa taifa hili, mhamasishaji mkubwa wa raia wa Zimbabwe kuzikwa katika eneo lingine lolote kando na makaburi ya mashujaa. Wito ni kuiomba familia – huyu sio wenu tena, ni kiongozi wa taifa. Ni kiongozi wa Afrika. Ni kiongozi duniani, Anastahili kupewa heshima anayoistahili . Kwahivyo atazikwa katika kaburi la kitaifa’,“ameeleza Mavhima.

Kwasasa mwili wa Mugabe umehifadhiwa katika Jumba lake la kifahari la Blue roof lililopo jijini Harare.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na familia, Mazishi ya Mugabe yatakuwa ni ya kifamilia na yatafanyika Kijijini Kutama siku ya Jumatatu au Jumanne, Na mwili utawasili kijiji hapo Jumapili usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents