Habari

Mazishi ya mwana kijiji aliyeuwawa kwa kushambuliwa na tembo (Video)

Wananchi pamoja na viongozi katika kijiji cha makuyuni wilayani Monduli Mkoani Arusha wameiomba serikali na mamlaka ya wanyama pori kuchukua hatua madhubuti katika kudhibiti wanyamapori wanaoingia katika makazi yao na kuwajeruhi na wakati mwingine kukatisha uhai wa raia .

Hayo yamesemwa Jumatatu hii na Mwenyekiti wa kijiji cha makuyuni juu Ngoyoo Measi wakati wa Mazishi ya marehemu Ester Mollel aliyeuwawa kwa kuvamiwa na tembo katika eneo la makuyuni juu Wilayani humo .

Kwaupande wake mtoto wa marehemu Elia Sangeti pamoja na mmoja kati ya watu waliowahi kujeruhiwa na wanyamapori na kusababishiwa majeraha ya kudumu wamesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya kuogopa kwakuwa mara nyingi wanyamapori huingia katika makazi
yao.

Sarafino Mawanja ni afisa wanyamapori katika Wilaya ya Monduli amesema wao kama mamlaka ya wanyamapori wamefanya jitihada mbalimbali katika kusaidia wananchi kutodhuriwa na wanyamapori ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wananchi walidhuliwa na kuwataka wananchi hao kuchukua tafadhari .

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita jumla ya watu 6 wamepoteza maisha kwa kudhuliwa na wanyamapori na takribani watu 7 wamepata majeraha ya kudumu katika kijiji cha Makuyuni Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents