Burudani ya Michezo Live

Mbabe wa kivita wa DR Congo ahukumiwa miaka 30 jela, ICC yadai hastaili kifungo cha maisha 

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, mbabe wa zamani wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Bosco Ntaganda, kwa makosa ya ukatili, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na kuwatumikisha watoto jeshini.

Image result for ICC Bosco Ntaganda

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Deutsche Welle, Ntaganda mwenye umri wa miaka 46, alikutwa na hatia Julai 18 kuhusiana na vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, vilivyofanyika wakati alipokuwa kiongozi wa kijeshi wa kundi la wapiganaji la Union des Patriots Congolais (UPC),-Umoja wa Wazalendo wa Congo, mashariki mwa Congo kati ya 2002 hadi 2003.

Image result for ICC Bosco Ntaganda

Wakati akisoma hukmu hiyo, jaji wa mahakama ya ICC Robert Fremr, amesema uhalifu aliohukumiwa Ntaganda, licha ya ukubwa wake na kiwango chake cha kulaumika, hakustahili kifungo cha maisha gerezani.

Mkuu wa Ntaganda, kiongozi wa chama cha UPC Thomas Lubanga, anatumikia kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kutiwa hatiani na ICC kwa kuandikisha na kutumikisha watoto jeshini.-

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW