Michezo

Mbabe wa Novak Djokovic atembeza kipigo kingine, atinga nusu fainali kwa kishindo

Mcheza tenesi kutoka Korea Kusini Chung Hyeon amefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Australian Open 2018.

Chung ametinga kwenye hatua hiyo baada ya kumtupa nje ya mashindano hayo Tennys Sandgren kwa seti 6-4 7-6 (7-5) 6-3.

Awali mchezaji huyu anayeshika nafasi ya 58 katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani hakupewa nafasi hata kidogo kufikia katika hatua hiyo huku akimtupa nje ya michuano hiyo kigogo Novak Djokovic Jumatatu hii kwa seti 7-6, 7-5, 7-6.

Chung Hyeon amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Korea Kusini kufika katika hatua kama hiyo ya michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents