Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Mbabe wa Tyson, Muhammad Ali amvulia kofia Joshua

Bingwa wa zamani wa dunia uzito wa juu katika mchezo wa masumbwi, Larry Holmes amesema kuwa kijana, Anthony Joshua atakuwa miongonini mwa mabondia bora kabisa wa muda wote siku za usoni.

Bondia Anthony Joshua

Holmes, ambaye ameshawahi kupigana na vigogo kama Mike Tyson na Muhammad Ali amesema bingwa huyo wa dunia wa WBA na IBF, Joshua atafikia hatua hiyo endapo ataendelea kuwa na  jitihada katika mchezo wa ngumi.

Bingwa wa zamani wa dunia uzito wa juu katika mchezo wa masumbwi, Larry Holmes

Bingwa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 67, amekiri kuvutiwa na kiwango kinachooneshwa na Joshua ambaye anatarajia kutetea mkanda wake Octoba 28 pale atakapo kabiliana na bondia, Kubrat Pulev kutoka Bulgaria katika uwanja wa Cardiff.

Holmes amekiambia chombo cha habari cha Sky kuwa “Nilipata ubingwa wa uzito wa juu wa dunia wakati nina umri wa miaka 30, lakini kijana huyu Joshua ameupata akiwa na miaka 27 pekee.”Amesema Holmes.

Larry Holmes ameongeza “Nafikiri anayonafasi nzuri ya yeye kudhihirisha kuwa bondia bora wa muda wote. Unapaswa siku zote kujiona wewe ni bora kuliko mwingine na kama ataendelea hivyo naamini atakuwa mkakamavu na kumfanya kujakuwa bondia bora.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW