DStv Inogilee!

Mbakaji sugu ajinyonga kwa blanketi akiwa gerezani Afrika Kusini

Mwanamume anayetuhumiwa kuwa mbakaji sugu nchini Afrika Kusini ,Sifiso Makhubo, amekutwa akiwa amefariki katika chumba chake gerezani.

rape_south_africa

BBC Swahili imeripoti kuwa Sifiso Makhubo, alikuwa anakabiliwa na mashtaka 122 ikiwa ni pamoja na mauaji na ubakaji . Makhubo alikutwa amejinyonga kwa kutumia blanketi katika chumba chake cha gerezani.

Makhubo anatuhumiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya Januari mwaka 2006 na Februari 2011.

Hadi sasa uchunguzi uliofanywa wa DNA katika waathiriwa waliodai kubakwa naye, ulithibitisha kuwa yeye ndiye alikuwa mbakaji.

SOURCE: BBC SWAHILI

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW