Michezo

Mbao FC yatuma salamu zavitisho Simba SC

Kuelekea mchezo namba 25 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba SC dhidi ya Mbao FC unotarajiwa kuchezwa leo siku ya Alhamisi majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza mwenyeji klabu ya Mbao imekiri mtanange huo utakuwa mgumu licha yakuwa na kila sababu ya kutoka na alama tatu muhimu.

Kikosi cha Mbao FC kikiwa katika mazoezi ya mwisho hapo jana kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Butimba

Mbao FC imeyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa nilazima watatoka na pointi tatu kwakuwa wao ndiyo wenyeji wa mchezo huo.

“Mechi itakuwa ngumu lakini sisi ndio wenyeji kwahiyo tuna kila sababu ya kushinda maana mcheza kwao hutunzwa. Karibuni mtutunze ili tuweze kuibuka na ushindi kwani ushindi huu ni wa Mwanza nzima”.

“Siku ndio leo ambapo vijana wenu tunajitupa Uwanjani kuumana na Simba SC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom. Jitokezeni kwa wingi CCM Kirumba kutupa hamasa vijana wenu ili kuhakikisha mnyama anakaa mapema karibuni tujenge historia”.

Mbao FC wamefanya mazoezi ya mwisho siku ya jana kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Butimba kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa duru la nne  wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Simba SC utakaopigwa leo Alhamisi kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents