DStv Inogilee!

Mbappe akiri “Nilishindwa kulala baada ya kufungwa na kutolewa kwenye michuano ya UEFA na Manchester United, Niliona kama uchawi” (+ Video)

Katika mojiano yake na kituo cha Telefoot cha nchini Ufaransa mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylin Mbappe amefunguka na kukiri ya kwamba alishindwa kulala kabisa baada ya kutolewa kwenye michuano ya UEFA na Manchester United katika hata 16 bora.

Akiongea kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwenye michuano hiyo Mbappe ameema:- ” Kwanza nilibaki nimeshangaa tu halafu nikaishiwa na maneno na baada ya hapo Sikuweza kulala na nadhani imekuwa sawa kwa kila mtu mwingine ambaye yuko hapa PSG”

Mbappe ameongeza :- ” Uwanja ulijaa mashabiki wetu tu na mashabiki walifanya kazi yao ya kushangilia, kweli ilikuwa hali ya kimiujiza, tuliharibu sherehe yetu wenyewe”

“Kuna watu wengi sana ambao wanatutukana, lakini bado ninaamini timu yangu, nina uhakika tutafanya kitu kizuri kwa klabu yetu pia na msaada wa mashabiki wetu, Natumaini kwamba wanaendelea kuwa nyuma yetu. “

https://twitter.com/telefoot_TF1/status/1104687647568613376

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW