Habari

Mbele ya Marais hawa, Museveni na Kagame wapeana mikono na kuahidi kumaliza uhasama

Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Museveni Kagame

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo na Angola waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Joto la kisiasa limekuwepo kwa takriban miaka mitatu sasa na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Image

Maafisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

“Tutashughulikia matatizo haya yote”. rais Kagame amewaambia wandishi habari baada ya kusaini makubaliano hayo.

Makubaliano ya leo yamefikiwa baada ya “jitihada zilizoidhinishwa na Angola kwa usaidizi wa DR Congo” kwa mujibu wa ikulu ya Angola.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kutilia mkazo kutatua mzozo wowote baina ya mataifa yao kwa njia amani shirika la habari nchini Angola, Angop linaripoti.

Uganda Rwanda: Mzozo wa kihistoria

Mnamo machi mwaka huu katika hotuba kwenye mkutano wa kitaifa, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameelezea kuwa chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na nchi ya Uganda ni la tangu miaka 20 iliyopita nchi ya Uganda ikitaka kuangusha utawala wake.

Rais Kagame amesema mgogoro huo ulishika kasi hivi karibuni kufuatia wananchi wa Rwanda wanaoingia nchini Uganda au kufanyia kazi nchini humo kushikwa na kuzuiliwa sehemu ambazo hazijulikani na kufanyiwa vitendo vya mateso huku akishtumu utawala wa Uganda kutoa nafasi ya ushirikiano kwa kundi la Rwanda National Congress linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa:

”RNC wanafanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya usalama vya Uganda.kilicho wazi ni kwamba Wanachokifanya ni kunyanyasa wanyarwanda ambao hawataki kuungana nao huku wakiwasingizia a kwamba wametumwa na utawala wa Kigali kuhujumu usalama wa Uganda na kuuwa wanyarwanda wa upinzani.Ni madai yasiyo na msingi.lakini haya yote yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliyopo baina ya serikali ya Uganda na kundi la RNC.”

Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake,shutuma ambazo Rwanda inakanusha.

Rais Kagame amesisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Katika ishara nyingine ya kuonekana ya kingia doa kwa uhusiano baina ya nchi hizo jirani, Mnamo Mei Uganda na Rwanda zilishutumiana kwa mauaji na utekaji nyara wa raia wa kutoka mataifa hayo mawili.

Kutokana na uhasama huu , Rwanda imeamua kufunga mpaka wake na Uganda wa Gatuna kwa usafiri wa bidhaa.

Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake,shutuma ambazo Rwanda inakanusha.

Rais Kagame amesisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents