Michezo

Mbeya City yamfungashia virago Kocha wake

Klabu ya Mbeya City FC imesitishwa mkataba na aliyekuwa kocha Mkuu, Kinnah F. Phiri ambaye alianza kandarasi ya kuitumikia timu hiyo Agosti 2 mwaka 2016.

Katika vikao vilivyokuwa vikiendelea hapo jana ndani ya klabu hiyo ya Jiji la Mbeya ni   muendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizo mbili toka mwezi julai mwaka huu  na hatimaye wamekubaliana kusitisha mkataba wa kazi na. Mwalimu Phiri aliyetokea katika timu ya Free State ya South Afrika

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo iliyoleta changamoto kubwa kunako ligi kuu ya Vodacom misimu miwili iliyopita inasema kuwa inamfungashia virago Kocha huyo sababu kubwa ikiwa ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yameipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha.

Huku Mbeya City ikitarajia kutangza kocha mkuu baada ya muda mfupi ujao ila kwa sasa timu itabaki chini ya usimamizi wa kocha msaidizi Mohamed Kijuso.

“Klabu inapenda kumshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu yetu, itaendelea kuuthamini na kuukumbuka na inaamini Kocha Phiri ataendelea kuwa msaada katika maendeleo ya timu yetu kwani amekuwa sehemu ya familia yetu”, zinasema taarifa kutoka katika mtandao wa Mbeya City.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents