Afya

Mbeya: Watu 9 wawekwa Karantini wakihofiwa kuwa na virusi vya Corona, Mkuu wa Mkoa azungumza haya

Mbeya: Watu 9 wawekwa Karantini wakihofiwa kuwa na virusi vya Corona, Mkuu wa Mkoa azungumza haya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema kuwa watu zaidi ya tisa kutoka Mataifa mbalimbali ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wamewekwa karantini chini ya ulinzi wa Mkoa wa huo baada ya kuhofiwa kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Taarifa hiyo imetolewa leo April 1, 2020, na Mkuu wa Mkoa huo na kusema kuwa watu hao wamewekwa karantini katika baadhi ya hoteli zilizo pembezoni mwa Mji kwa muda wa siku 14 na wanahudumiwa na wahudumu ambao wamepata mafunzo maalumu.

“Tulichokifanya katika mipaka ni kuhakikisha wale wageni wote wanaoingia, wanapimwa kwanza na kukaa karantini kwa siku 14 kwa gharama zao, mpaka sasa hatuna kesi yoyote lakini tuna watu zaidi ya tisa, ambao wametengwa kwenye karantini hizo” amesema RC Chalamila.

Chanzo Eatv.tv

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents