Habari

Mbeya: Zaidi ya vibanda 2000 vyateketea katika soko lililoungua

Zaidi vibanda 2000 Katiba ya vibanda 3600 vilivyopo katika soko la biashara la Sido mjini Mbeya vyateketea kwa moto na mali zote zilizokuwepo kwenye vibanda hivyo zimeungua.

Katibu wa Soko hilo Lameck Ngogo amemuambia mwandishi wa habari wa TBC 1 kuwa moto huo umeteketeza vibanda vyote vilivyokuwa vimejengwa kwa mbao na kusababisha hasara kubwa.

“Hapa mahali palikuwa ni maduka kama unavyoona zote zimeteketea na hapa palikuwa na stoo kama unavyoona huyu jirani yangu, lakini mpaka saivi hatuna la kusema,” alisema mmoja ya wafanyabiashara wa soko hilo.

“Soko la Sido linawafanyakazi 3136 vibandavilivyopona ni vya kontena vibanda 2000 na kitu vyote vimeteketea kwa moto na mali zote zimeungua hatuwezi kutoa tathmini kuwa ni mali za kiasi gani zimepotea lakini yule aliyefanikiwa kuokoa mali asilimia 60 zilikuwa zinapotea na vibaka,”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents