Soka saa 24!

Mbivu na mbichi kuhusu Jose Mourinho kujulikana saa 48 zijazo

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward saa 48 zijazo jijini London kabla ya bodi kufanya mkutano wake hapo kesho siku ya Alhamisi.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho

Endapo mkurugenzi huyo, Woodward atafikia muafaka wa kumbakiza Mourinho ndani ya United pindi watakapo kutana basi Mreno huyo atakuja na ajenda ya usajili wa dirisha la mwezi Januari kwenye mkutano wa bodi hiyo.

Mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward

Kwamujibu wa The Sun limeandika kuwa kubaki kwa Mourinho kwenye klabu ya Manchester United kutajulikana baada ya kukutana na Woodward saa chache zijazo.

Mourinho anahitaji kufanya usajili wakati wa dirisha lijalo ili kuimarisha kikosi chake wakati tayari mpaka sasa ameshatumia pauni milioni 350.

Alhamisi hii bodi ya klabu ya Man United inatarajia kufanya mkutano na kujadili hatma ya Mourinho na maandalizi ya mwaka mppya unaokuja 2019.

Licha ya kutokuwa na matokeo mazuri lakini bado Mourinho amekosa malewano na baadhi ya wachezaji wake akiwemo Pogba aliyemtaka kocha wake kutumia mfumo wa kushambulia zaidi pindi wanapokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW