Habari

Mbongo atangaza kununua Liverpool FC

Mfanyabiashara nchini Tanzania, Bw. Suleiman Nassor ametangaza nia ya yeye na familia yake iliyopo Oman na Dubai kutaka kununua timu ya Liverpool FC iliyopo katika ligi kuu ya Uingereza.

 

Timu ya Liverpool FC inasadikika kuwa ni paund milioni mia tatu.

Nassor alitangaza nia hiyo ofisini kwake Kinondoni Dar es Salaam huku akitaja sababu hasa ni kuwa mtoto wake, aendaye kwa jina la Fahad Suleiman Masoud,ambaye anachezea Liverpool Academy, amechangia kwa kiasi kikubwa sana kutoa hamasa kwa familia hiyo kutaka kuimiliki timu hiyo.

Amesema kwa sasa familia iko katika utaratibu wa kuzungumza na benki tofauti ili kuhakikisha mikataba na ununuzi unaenda vyema.

(picha kwa hisani ya fullshangwe)

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents