Habari

Mboni Masimba Anakuja Na “Mboni Talk Show” Ndani Ya EATV


Mwanadada mjasiriamali Mboni Masimba leo asubuhi ametangaza kuja na kipindi chake “Mboni Talk Show” ambacho kitajadili na kutimiza ndoto za vijana wa kada mbali mbali za kijamii za Tanzania kupitia fursa itakayotokana na kipindi hicho.
Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli Serena jijini leo Mboni alisema Kipindi chake kitakuwa na madhumuni makuu 5 ambayo aliyataja kuwa ni pamoja na Kuburudisha, kuelimisha, Kuonya, Kuadibu na Kuelekeza.

Akiendelea Mboni alisema kipindi chake kitakuwa na awamu tatu ambazo ni pamoj na ufunguzi wa kipindi, maswali kutoka kwa mtangazaji kwenda kwa wageni waalikwa, Maswali kutoka kwa hadhira kwenda kwa wageni, my dreams come true na tamati.

Naye mkurugenzi wa utayarishaji bwana George Tyson akiongea kama muongozaji katika utengenezaji wa kipindi hicho cha Mboni Talk Show alisema wao kama watayarishaji watazingatia mada, ubunifu, uchangamfu, utoaji wa fursa za kuibua na kuendeleza vipaji vipya pamoja na kuzawadia haja ya moyo. Pia alibainisha kuwa wanategemea kipindi hicho kuwa kipindi bora kwani watazingatia ubora ambao umewafanya wao kupata nafasi ya kuonyesha kipindi hicho katika kituo cha luninga cha East Africa Television.

Naye mkurugenzi wa program wa kituo cha East Africa Television bibie Sophia Mng’anya alisema wao kama kituo namba moja cha luninga kwa vijana wamekubaliana na Kampuni ya Chocolate Princes kurusha kipindi hicho baada ya kuridhika na ubora wa kipindi hicho cha Mboni Talk Show ambacho kinatarajiwa kuanzakuonekana Tarehe 31, Mei majira ya saa 3 za usiku huku kipindi kikichukua lisaa moja kuruka hewani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents