Bongo Movie

Mboto atinga kwa Mzee Majuto

Mchekeshaji Haji Mboto maarufu kama Mboto, ameamua kutinga jijini Tanga kumjulia hali mchekeshaji mwenzake King Majuto aliyekuwa amelazwa hospitali kwa muda wa siku tatu baada ya upasuaji wa hernia (ngiri).

Kufuatia taarifa zisizo za kweli kuzagaa katika mitandao kuwa mchekeshaji huyo mkongwe amefariki dunia, Mboto ikamlazimu kufika nyumbani kwa mzee huyo na kufahamu kinachoendelea.

“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mzee majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizur na sivyo kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunae. Kwa sasa mzee ni mzima nipo nae Tanga,” ameandika Mboto kupitia mtandao wa Instagram.

Mboto na King Majuto wamekuwa wakifanya kazi ya uchekeshaji siku nyingi na kuonyesha kuwa tasnia hiyo ina mafanikio na kuweza kuibua wachekeshaji wengine wapya katika sanaa hiyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents