Afya

Mbowe ajiweka Karantini baada ya mtoto wake kuthibitishwa kuwa na Corona “Rais Magufuli alinipigia simu kunipa pole”

Mbowe ajiweka Karantini baada ya mtoto wake kuthibitishwa kuwa na Corona "Rais Magufuli alinipigia simu kunipa pole"

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amejiweka karantini siku chache baada ya kutangaza kuwa mwanaye Dudley amepata maambukizi ya #COVID_19.


Mbowe amesema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na hivi sasa yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama naye ana Virusi hivyo.

Akiongea na Clouds Media Mbowe amesema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na #CoronaVirus ili aliokutana nao pia wawe salama.

Aidha, Mbowe ameeleza kuwa mkakati wa pamoja unahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona ambao amesema ni suala ya kitaifa.

Mbali na hilo Mbowe amethibitisha kuwa Rais Magufuli alimpiga simu na kumpa Pole “Mh. Rais alinipigia simu na kunipa pole”

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents