Habari

Mbowe asiporipoti tutamfuata – Kamanda Sirro

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe asipofika bila kutoa taarifa yoyote atatafutwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.

Hayo ameyaeleza Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro Ijumaa hii wakati akizungumza na wanahabari nje ya kituo hicho baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Oparesheni ya dawa za kulevya bado inaendelea na kuanzia sasa hatutaruhusu mkusanyiko wa wananchi karibu na kituo cha polisi hiki watakaoonekana watashughulikiwa na asije akalaumiwa Kamishina Sirro kwa kuwa tayari nimeshatoa taarifa.”

Waandishi walipo muhoji kuhusu watu wangapi waliofika kituoni hapo kufikia siku ya leo alisema “watu waliofika kituoni hapa niliowatambua ni wanne tu,” waandishi walipotaka kuyatambua majina hayo alidai kuwa hawezi kuyataja.

Aidha Kamanda Sirro amesema askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji walilala polisi kwa kuwa bado upelelezi dhidi yao unaendelea.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents