Habari

Mbunge aibua hoja kuhusu serikali kujenga viwanda 100 kila Mkoa

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema kiwanda kina tabia ya binadam kinapokosa mazingira mazuri na wezeshi kinaweza kufa hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa anajenga mazingira wezeshi ikiwemo kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya viwanda.

Manyanya ameyasema hayo leo bungeni Mjini Dodoma, Wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mariam Msabaha alieuliza,

Serikali imekuwa ikieleza kuwa inajenga viwanda 100 kila Mkoa na Mkoa wa Morogoro ulikuwa ni moja ya mkoa wenye viwanda vingi enzi za Mwalimu lakini hivi sasa viwanda vingi vimekufa na vimegeuka kuwa magodouni,  Je? serikali haioni umuhimu wa kufufua viwanda kwanza vilivyokufa na hapo ndipo ije na wazo la kujenga viwanda vipya?

“Ahsante Mwenyekiti kwanza tunamshukuru kwa ufuatiliaji ni kweli kwamba serikali iko serious na kuona kwamba viwanda vingi vinajenga Tanzania  hasa katika kuongeza thamani ya mazao ya wananchi tulionao jirani tuliyonayo ndani  na viwanda hivyo kama nilivyokuwa nikisisitiza kila wakati viko katika ngazi za aina mbalimbali,kuna viwanda vidogo sana, viwanda vidogo na viwanda vya kati kwahiyo wananchi wenye mitaji midogo wanaouwezo wa kuanzisha viwanda kulingana na hali inayowezekana,” amesema Mhandisi Manyanya.

“Sasa suala la viwanda vya zamani ambavyo havifanyi kazi kwanza tutambue kwamba kiwanda kina tabia sawa na binadam kiwanda kinapokosa mazingira mazuri na wezeshi kinaweza kufa sawa na binadam anavyokufa kwahiyo ni wajibu wetu sisi kuhakikisha kuwa tunajenga mazingira wezeshi ikiwemo kupunguza  au kuondoa kabisa vifo vya viwanda na hiyo ndio kauli mbiu na hiyo ndio jitahada inayofanyika ndio maana unakuta jitihada mbalimbali zinaendelea kwahiyo Morogoro ni sehemu moja wapo ambayo tumeshaitembelea. Nizidi kuwaomba Watanzania msitishike nimetembelea zaidi ya viwanda nilivyotembelea asilimia 90 vinaendeshwa na sisi Watanzania wenyewe kwahiyo tujitoe hata sisi wabunge tuanzishe viwanda kadiri inavyowezekana kulingana na mahitaji ya maeneno yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents