Habari

Mbunge aihoji serikali nafasi ya Zanzibar katika Jumuiya za Kimataifa

Naibu wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,Dkt. Susan Kolimba amesema kuwa serikali imekua ikihakikisha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inashiriki kikamilifu masuala yote ya Kimataifa.

Kolimba ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swala la Mbunge wa Wingwi, Juma Kombo Hamad aliyehoji

Je, Zanzibar ina nafasi gani katika Jumuiya za Kimataifa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

“Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mabadiliko yake masuala ya mambo ya nje yapo chini ya mamlaka ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali imekua ikihakikisha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inashiriki kikamilifu masuala yote ya Kimataifa masuala hayo ni pamoja na ziara za viongozi na mashirika mbalimbali za Kimataifa zinazofanyika hapa nchini, ziara zinazofanya na viongozi wa Kitaifa kwenye nchi mbalimbali , mikutano ya mashirika na Taasisi za Kimataifa na kikanda na mikutano ya pande mbili na Zanzibar kuwa mwenyeji wa mikutano ya Kimataifa,” amesema Dkt. Kolimba.

“Aidha viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa wakiongoza ujumbe wa nchi kwenye mikutano mbalimbali ya Kimataifa kwa mfano kwa mwaka 2017/018 serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeshiriki katika mikutano ipatayo 11 ya mashirika na Taasisi mbalimbali za Kimataifa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents