Tupo Nawe

Mbunge ajitosa kumvua Mbowe uenyekiti CHADEMA, “Muda wake umefika kuwaachia wengine”

Mbunge wa Ndanda kupitia tiketi ya CHADEMA, Cecil Mwambe, ametangaza nia ya kutaka kuchukua nafasi ya Uenyekiti Taifa wa CHADEMA.

Kwa sasa chama hicho Mwenyekiti wake ni Freeman Mbowe, Na kwa mujibu wa Katiba yao wanatakiwa kufanya uchaguzi wa ndani ya chama.

Hivi karibuni, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilikitaka Chadema kuwasilisha maelezo katika ofisi yake kwa kile alichoeleza ni kukiukwa kwa Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kusogeza mbele uchaguzi wa viongozi wake.

Katika barua hiyo Msajili aliagiza maelezo hayo kuhusu sababu za kuahirishwa kwa uchaguzi huo kuwasilishwa katika ofisi hiyo kufikia Oktoba 7, mwaka huu (leo) saa tisa na nusu mchana.

Akihojiwa na gazeti la Nipashe, Mbunge huyo, amesema umefika wakati wa chama hicho kupata mwenyekiti mpya, kwamba ameamua kugombea nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa ana sifa za kuongoza.

Tunamshukuru Mwenyekiti wetu kwa mambo mengi mazuri aliyokifanyia chama chetu na imefika muda sasa kuwaachia wengine,” amesema Mwambe.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Kanda ya Kusini na mjumbe wa Kamati Kuu, alidai kuwa ana uwezo wa kuongoza chama hicho, Baada ya kupata uzoefu wa kuongoza ukanda huo, hivyo sasa anaona anatosha kwa nafasi ya Taifa ndani ya chama hicho.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW