Burudani ya Michezo Live

Mbunge aliyewabeza wahudumu wa ATCL aomba radhi bungeni, Spika Ndugai ampongeza

Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Husna Mwilima leo Novemba 14, 2019 amewaomba radhi Watanzania na wanawake wenzie, Kufuatia kauli yake aliyoitoa Novemba 7 mwaka huu Bungeni, Ambapo alisema kuwa wahudumu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania hawana mvuto.

Image

Mwilima ameomba radhi mapema leo Bungeni kwa kusema “Naomba radhi Watanzania na Wanawake wenzangu, Naomba nichukue nafasi hii Mhe. Spika kuomba radhi hasa kauli yangu niliyoitoa hapa bungeni,“.

Kufuatia tukio hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amempongeza Mbunge huyo kwa kumuita mtu mwenye busara na muungwana kwa kuomba radhi.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW