Habari

Mbunge aomba namba za Mawaziri kuwekwa hadharani kama za Ma-RPC (+video)

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Jaku Hashimu Ayoub ameiomba serikali kuweka namba za Mawaziri hadharani kama ilivyo kwa Makanda wa Polisi wa Mikoa (Ma-RPC).

Jaku ametoa ombi hilo leo, Juni 26, 2018 Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka Wabunge na wananchi wakitaka kuwapigia wawapate huku alilalamika kuwa kuna namba za Mawaziri wengine hazipatikani.

“Hizo kanuni nani alizisimamia ili hao Mawaziri ambao wamo humu ndani hawapokei simu zikiwemo za Wabunge mbali na za wananchi ili hatua zichukuliwe ikiwa namba za Ma-RPC ziko hadharani na ziko katika mtandano, sababu gani zinasababisha Mawaziri namba zao zisiwe hadharani. Ni lini namba za Mawaziri zitatangazwa hadharani ili wananchi na wabunge wakiwapigia wapokee?,” alihoji Jaku.

Akitoa majibu ya swali hilo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amemshangaa Mbunge Jaku aliyelalamika namba za Mawaziri kutopatikana kwenye simu wakati amedai namba zao hazipo hadharani “Analalamika kwamba Mawaziri hawapati kwa simu lakini wakati huo analalamika namba zao haziko hadharani sasa hao ambao huwapati kwa simu ni wapi kama simu zao huna? alihoji Mkuchika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents