Habari

Mbunge kutoka CCM ashindwa kufukuzana na ‘Speed’ ya Rais Magufuli, Akataa kugombea tena uchaguzi mkuu 2020

Mbunge wa Rorya kwa tiketi ya CCM,  Lameck Airo, amesema kuwa hatogombea tena ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao 2020 na badala yake atawaachia vijana wapambanie nafasi hiyo.

Mhe. Airo ambaye kwasasa yupo katika ziara jimboni mwake, amesema  tayari amewasilisha taarifa hiyo kwenye chama chake juu ya kusudio lake na kwamba wamekusudia kuwa mchakato wa uchaguzi utakapoanza, watahakikisha Jimbo la Rorya linaongozwa na vijana shupavu na wenye sifa.

Mbunge huyo ambaye amekuwa madarakani kwa mihula miwili, amesema atatimiza ahadi zake zote alizoahidi wakati wa kampeni za mwaka 2015 na kwamba kazi aliyofanya kwa miaka tisa, itabaki kuwa historia.

Kwa upande mwingine, Katika ziara hiyo pia alimkabidhi Diwani wa Kata ya Nyamtinga, Chacha Nyambaki (CCM) mabati 200, mifuko ya saruji 100 na Sh milioni moja kumalizia uezekaji wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule zilizoezuliwa paa kwa upepo.

Kama mbunge nitahakikisha kwa kipindi kilichobaki cha mwaka mmoja  kabla ya Uchaguzi Mkuu, ahadi zangu zote zinatekelezwa ili atakayerithi nafasi hii, chama kisipate shida kumnadi ifikapo 2020. Najua mwezi ujao nchi itakuwa na uchaguzi mdogo, chama na mimi binafsi tunataka tuone  Rorya tunaikabidhi kwa vijana, hivyo nawataka wajiandae. Pia kina mama jitokezeni kugombea nafasi mbalimbali, tumechoka kuona sura zile zile miaka yote.  Wale mnaosubiri kila muda kupewa nafasi za viti maalumu nanyi nendeni mkagombee, hivi sasa tunawapa wale ambao hawajawahi kupata ili nao wapate uzoefu,” amesema Airo.

Chanzo: Mtanzania

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents