Tupo Nawe

Mbunge Lissu aibuka mwaka 2019 na waraka mzito, Rais Magufuli na Diamond watajwa (Video)

Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha upinzani Chadema, ameufungua mwaka 2019 kwa kuandika waraka mzito ambao ndani yake umewataja Rais Magufuli pamoja na muimbaji Diamond Platnumz.

Mwanasiasa huyo ambaye alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 Septemba 7 2017 na watu wasiojulikana, Jumapili hii Januari 6 2018 ameendelea kulihoji Bunge na Serikali ya Tanzania kutogharamia matibabu yake na pia kukwama kwa uchunguzi na kukamatwa kwa watu waliomshambulia.

Katika kipengele alichotajwa Diamond, Lissu amelilalamikia Baraza la Sanaa Taifa BASATA kwa madai kwamba limeshindwa kufanya kazi kwa weledi na kubaki kuwafungia wasanii.

Lissu amemtaja pia Rais John Magufuli akihoji sababu za kutomjulia hali ya afya yake. Hata hivyo, baada ya tukio hilo, Rais Magufuli alimtuma Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwenda Nairobi alikokuwa amelazwa kumjulia hali na kumpa salamu za pole.

Mbali na kudai gharama za matibabu ya Bunge, Lissu amelalamika kutotembelewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wala watumishi wa Bunge licha ya kuahidiwa.

“Hadi ninapoandika maneno haya, bado Spika Ndugai hajatimiza ahadi yake hiyo. Hakuna mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge, au afisa yeyote wa Bunge, aliyefika hospitalini kuniona na kunijulia hali,” amesema.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW