Habari

Mbunge mpya wa CUF, Bi Hindu Mwenda afariki dunia

Mmoja kati ya wabunge 8 wateule kutoka Chama cha Wananchi CUF Bi. Hindu Hamis Mwenda amefariki dunia.

Bi Hindu Mwenda enzi za uhai wake

Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama hicho Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki katika hospitali ya taifa Muhimbili jana jioni alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Taarifa hiyo haijaeleza kwa undani chanzo cha kifo hicho, lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa baadaye.

Wabunge hao wapya wa viti maalum pamoja na marehemu, waliteuliwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada waliokuwa wakishika nafasi hizo kuvuliwa ubunge kutokana na kuvuliwa uanachama na hivyo kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

Mwanzoni mwa wiki hii Spika wa Bunge Job Ndugai alitamka kuwa wabunge hao wapya wataapishwa katika kikao cha kwanza cha mkutano ujao wa bunge utakaoanza Septemba 5 mwaka huu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents