Habari

Mbunge Musukuma amtaja mwanasiasa wa upinzani anayemvutia, adai wabunge wengi wanavuta bangi

Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku (Musukuma) bado anakazia kauli yake ya kuitaka serikali  iruhusu biashara ya bangi na mirungi.

Image result for musukuma
Musukuma

Musukuma amesema kuwa bangi ni nzuri kuliko pombe kwani mtu akivuta ana kuwa na nguvu za kufanya shughuli zake huku akidai kuwa hata bungeni kuna viongozi wakubwa wanatumia bangi.

Mule ndani (bungeni) kuna viongozi wakubwa tu wanavuta bangi, na wakija mule wanakuja na mizuka yao, nilimuomba Spika niwataje akanikataza,” amesema Musukuma kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV.

Kwa upande mwingine, Musukuma amemtaja Prof. Lipumba kama ndio kiongozi wa upinzani anayemvutia kwenye siasa za upinzani nchini Tanzania.

“Mwanasiana wa upinzani anayenivutia ni Lipumba anajua hesabu za kuvuruga vyama nampenda sana, Lipumba yeye na Sakaya ni mabingwa wa kutibua siasa anajua kupiga hesabu za kuchekecha vyama, na mimi katika maisha yangu nataka niwe kama yeye.”ameeleza Musukuma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents