Habari

Mbunge wa CUF aipongeza serikali kwa kukuza uchumi

Mbunge wa Viti Maalum, Chama cha Wananchi(CUF), Rukia Kassim amepongeza juhudi za Serikali katika kukuza uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la Taifa.

Mhe. Rukia ameyasema hayo leo Bungeni, Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19.

“Naipongeza Serikali kwa hatua za kukuza uchumi hasa ukuaji wa Pato la Taifa unaotarajiwa kuwa asilimia 7.2”, alisema Rukia.

Naye Mbunge wa Urambo,Magreth Sitta ameipongeza Serikali kwa kupendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike.

“Mheshimiwa Spika hatua hii ya kusamehe kodi hiyo itapunguza bei ya taulo hizo ambayo itawafanya wanafunzi wa kike kuzipata kwa bei nafuu na kuwawezesha kuhudhuria masomo kwa muda wote wa masomo ikilinganishwa walivyokuwa wakishindwa kufanya hivyo wakiwa katika siku zao kwa kukosa taulo”,alisema Mama Sitta.

Akichangia kwenye bajeti kuu ya Serikali, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba amesema kuwa anampongeza saa Rais John Pombe Magufuli kwa kujenga miradi mikubwa miwili ya Standard Gauge naye Umeme wa Stiegler’s Gorge.

“Historia itamwandika Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya hasa kwa ujenzi wa miradi mikubwa nchini, ule wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) na ule umeme wa Stiegler’s Gorge”, alisema Serukamba.

Wabunge wanaendelea kuchangia bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambayo iliwasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents