Habari

Mbunge wa Kenya Johanna Ng’eno, akamatwa kwa kutoa maneno yaliyoelezwa kumtusi rais (+Video)

Mbunge mmoja wa Kenya amekamatwa kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wikendi iliyopita, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Johanna Ng’eno anatuhumiwa kwa kutumia maneno ya matusi kumdhalilisha rais, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Nation inayonukuu ripoti ya polisi.

Kanda ya video inayomuonesha mbunge huyo akizungumzia mgogoro kati ya rais Kenyata na naibu wake William Ruto imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii.

Mbunge huyo anasikika akimwambia rais avunje serikali ikiwa ameshindwa kufanya kazi na bwana Ruto.

Hali ya taharuki ilishuhudiwa wakati wa kukamatwa kwa mbunge huyo wa Emurua Dikirr, katika eneo la bonde la ufa huku tukio hilo likioneshwa moja kwa moja katika ukurasa wake wa Facebook.

Baada ya kukamatwa kwa bwana Ng’eno, naibu wa rais aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema “viongozi wanapaswa kujizuia na kuepuka kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wakenya wengine”

https://www.instagram.com/p/CE4JzU9jyLe/

https://www.youtube.com/watch?v=RqlNWL0C0rE

https://www.youtube.com/watch?v=XAnPUaqvJQQ

https://www.youtube.com/watch?v=tOGkBgOAcWA

https://www.youtube.com/watch?v=f7m-ZaiwKYQ

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents