Habari

Mbwa Roboti wajiunga na mazoezi ya jeshi la Anga la Marekani (+Video)

Jeshi la anga la taifa la Marekani limefanya mazoezi na Mbwa Roboti ambao wanatarajiwa kuja kutumika katika vita siku za usoni.

Robot dogs join US Air Force exercise giving glimpse at potential  battlefield of the future - CNN

Kikosi cha anga (C-130) cha jeshi la Marekani, kimeeleza kuwa Mbwa hao ambao ni Roboti walitoka nje ya ndege kukagua kama kuna hatari yoyote kabla ya binadamu kushuka kwenye uwanja wa vita, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa habari zilizotolewa na Jeshi la anga Septemba 3 mwaka huu 2020.

https://www.youtube.com/watch?v=-Dvqj2JzRVA

Mbwa Roboti ni moja ya jaribio la jeshi la Marekani ambalo linaitwa Advanced Battle Management System (ABMS). Hutumia mashine maalum katika kukusanya taarifa na kuzifanyia uchambuzi wa haraka wa data kugundua na kukabiliana na hatari itakayoikabili jeshi la Marekani na hivyo kuwezesha mashambulizi ya makombora ama zana nyingine.

Dr. Will Roper talks Acquisition Reform - YouTube

Katibu msaidizi wa jeshi la anga la Marekani, Dr. Will Roper amesema kuwa siku za usoni katika uwanja wa Vita wanajeshi watakabiliwa na changamoto za taarifa kutokuwa za uhakika ili kutathimini.

Robot dogs join US Air Force exercise giving glimpse at potential  battlefield of the future - CNN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents