Michezo

Mbwana Samatta aingia orodha ya 3 bora ya CAF

Mshambuliaji wa Taifa Stars ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbwana Samatta ametangazwa katika orodha ya wachezaji watatu bora na shirikisho la soka la Afrika CAF wanaocheza soka barani Afrika.

samatta3-e1437380737934

Samatta anashindana na wachezaji wengine wawili Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel na Kipa machachari wa TP Mazembe ya DR Congo Robert Kidiaba.

Mshindi atachaguliwa na makocha wa timu za taifa na kutangazwa katika dhifa maalum Januari tarehe 7 mwakani.

CAF ilikuwa imewataja wachezaji 37 katika orodha ya awali lakini wakachuja hadi 10 mwezi uliopita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents