Burudani ya Michezo Live

Mbwana Samatta huyoo Uingereza

Muda wowote kuanzia sasa Mshambuliaji hatari wa klabu ya KRC Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta huwenda akatambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa timu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Image result for Samatta to Aston Villa

Mbwana Samatta

Hii leo vyombo mbalimbali vya habari duniani vimekuwa vikiandika usajili huu wa kijana wa Tanzania kutua Aston Villa kwa dau la pauni milioni 10.

Kwa muda mrfefu Watanzania na Wanaafrika Mashariki wamekuwa wakitamani kuona nyota huyo mwenye umri wa miaka (27) akitua Premier League.

Bosi wa Aston Villa, Dean Smith amethibitisha kuwa klabu inahitaji kuongeza nguvu ya kikosi baada ya changamoto walizopata katika mzunguko wa kwanza, “tunalifanyia kazi hilo muda wote, ninafikiri tutakamilisha kabla ya Jumapili“, alisema wiki iliyopita.

Smith anahitaji mshambuliaji atakayeleta mabadiliko ndani ya timu hiyo inayoshika nafasi ya 18, baada ya kuumia kwa nyota wao Mbrazil Wesley.

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW