AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Mbwana Samatta, msimu ujao 2016/2017 kucheza Europa League

May 29, Nahodha wa timu ya taifa Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye anachezea klabu ya KRC Genk ya Inchini Ubelgiji ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).

yq2s

Kwa matokeo hayo, KRC Genk imefuzu Europa League kwa ushindi wa jumla wa 5-3, baada ya Ijumaa iliyo pita kufungwa 2-0 ugenini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi ya mwisho ya Europa League nchini Ubelgiji.
Samatta alikuwa ana mchango wake katika tiketi ya Europa League kwa KRC Genk, alifunga bao moja na kusababisha penalti huku akicheza kwa kiwango kizuri.

KRC Genk wataanzia katika hatua ya mtoano na kama watafuzu ndio watapangwa katika hatua ya Makundi ya Europa League, makundi ambayo yatachezeshwa droo hivyo inaweza ikatokea bahati Kwa KRC Genk ya Samatta kupangwa hata na klabu kubwa kama Man United endapo itafuzu mechi yake ya mtoano.

Related Articles

Check Also

Close
Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW