Bongo Movie

Mbwembwe za Black Sunday

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

 

Eneo la Mlimani City upande wa jumba la sinema Cineplex juzi usiku lilibadilika na kuwa Hollywood kwa muda baada ya ma celeb wa kibongo kufurika ukumbini hapo katika tukio la kwanza la kuzindua filamu ya Black Sunday. [Exclusive Videos]


Filamu hiyo ambayo imechezwa na Kanumba Steven na yusuf Mlela ilizinduliwa jana kwa mbwembwe za hali ya juu baada ya washiriki pamoja na wadau mbalimbali wa filamu za kibongo kualikwa na wengine kulipa kiingilio ili kuona uzinduzi huo wa kihistoria katika tasnia ya filamu Tanzania.

Mandhari ya eneo hilo la sinema ilibadilika pale ilipofika mida ya saa mbili usiku ambapo wageni mbalimbali waalikwa walifika na kuteremshwa katika zuria jekundu. lililokuwa maalum kwa ajili ya wandaaji, wacheza filamu na wageni waalikwa ambao walipokelewa na kupigwa picha pamoja na kufanyiwa mahojianona waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari.

Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bwana Miraji Kikwete ambaye aliwasili mida ya saa tatu na nusu na kupokelewa na Mkurugenzi wa kampuni ya burudani (pili pili entertainment) bwana Sameer Srivasta ambao ndio watengenezaji wakuu wa filamu hiyo na wadhamini wa tukio hilo la uzinduzi huo wa filamu Black Sunday.

Baadhi ya wageni mashuhuri walioalikwa na kujitokea katika uzinduzi huo ni pamoja na Ally remtullah, Sylvia Shally, Vincent Kigosi Ray, Zam Zam Rashid, Dr Cheni, mtangazaji wa TBC international, Ruge Mutahaba na Baby Madaha.

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

Black Sunday Premiere Steve Kanumba

{hwdvs-player}id=1164|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1157|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1158|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1159|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1163|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1160|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1162|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1161|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents